Social Icons

Thursday, 21 November 2013

JE BABA WA TAIFA ALIONA NINI KUHUSU RASILIMALI ZETU.Hebu turudi nyuma enzi na uhai wa Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikwisha tabiri majanga ambayo yanaweza kuwapata viumbe wa porini ikiwa binadamu ataendelea na utaratibu wa maisha yake bila ya kufikiria juu ya kizazi kijacho na wala viumbe wa porini kama hawa Tembo.Katika Tamko la Arusha maarufu kama"Arusha manfesto" Baba wa Taifa alitoa wito wa kulinda maliasili na rasilimali zetu, mpaka leo bado unabeba ujumbe mzito na kuwa na jina tu kwani hifadhi zetu ziko hatarini kupoteza umaarufu wake.

Katika tamko hilo Baba wa Taifa alisema

- Waafrika wote kuhakikisha kuwa wanyamapori wanaendelea kuwepo.

- Pamoja na wanyamapori kuwa vivutio, ni sehemu ya rasilimali ya maliasili muhimu kwa maisha yetu wote.

- Tunapokubali kuchukua dhamana ya kuhifadhi wanyamapori,tunatamka kwa dhati kwamba tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha vizazi vijavyo vitanufaika na urithi huu mkubwa.

-Uhifadhi wanyamapori na maeneo yao unahitaji maarifa ya kitalaam,watumishi walioelimishwa ,fedha,na hivyo tutatarajia kupata ushirikiano wa mataifa mengine.

- Madhara ya kutoweka rasilimali hii muhimu sio kwa bara la Afrika tu bali ni kwa dunia nzima.

No comments:

Post a Comment