Social Icons

Wednesday, 27 November 2013

JE TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA WENZETU? NYOKA NA KONOKONO WAMEKUA TIBA MBADALA KWA WATU WENGI NCHI ZA ULAYA NA ASIA


Nchini  Tanzania wapenzi wa kusingwa maarufu kama “massage”wamezoea kufanyiwa huduma hiyo na binadamu wenye mikona laini,lakini hali ni tofauti huko nchini  Indonesia ambapo hivi sasa huduma hiyo imekuwa ikitolewa na nyoka na konokono.
Wakati huo  Tanzania, nyoka akiendelea  kuwa adui mkubwa wa banadamu na konokono kuonekana mdudu anaetia kinyaa kwa baadhi ya watu,nchini  za China na Japan wanyama hawa wamekuwa wakitumika kama mboga na ewakati mwingine wamekuwa ni rafiki wa binadamu kwani wengi wao hufugwa na binadamu.
Ukistaajabu ya musa utayaona ya Firauni,kwani katika nchi za Ulaya miezi kadhaa iliyopita watu mbalimbali wameanza kupokea tiba kutoka kwa wanyama hao ikiwemo huduma ya kukanda na kupodoa uso (facial) inayotolwa na konokono na kusinga (massage) inayotolewa na nyoka.
Facial ya konokono
Kwa wengi wetu konokono ni mdudu mpole zaidi kuliko wadudu wengine wanaopatikana majanini,lakini nchini Japan wataaalamu wamegundua kuwa lami (uteute) anaotoa mdudu huyu ni tiba nzuri kwa ngozi ya binadamu, baada ya kutumika kwa miezi kadhaa nchini Japan sasa tiba hiyo imeanza kupendwa barani Ulaya,kama watu wanavyomiminika katika saluni moja iliyopo East Midland nchini Uingereza.
Matibabu hayo yanahusisha konokono kuanzia watatu ambao huwekwa juu ya uso wa binadamu na wao huanza kuzunguka maeneo mbalimbali ya uso huo,yamekuwa yakiongeza uwingi wa watu katika saluni za maeneo mbalimbali ya nchi za Ulaya.
Wataalamu hao wa facial ya konokono akiwemo DK Sunil Chopra wanasema kwamba katika matibabu hayo huwa wanahakikisha kwamba konokono anatembalea kila sehemu ya uso wa binadamu isipokuwa maeneo yam domo,macho na pua.
Kwa mujibu  wa mmiliki wa Simply Divene Saloon iliyopo Corby katika mji wa Northamptonshire nchini Uingereza,Diane Gower matokeo ya tiba hiyo inayogharimu kiasi cha dola 50 sawa na Sh 80,000.huonekana  papohapo na kwamba wadudu hao hutoa kamasi zenye protin muhimu kwa ngozi ya binadamu.
Anasema  “mwanzoni kwa mteja wa  kwanza huwa  wanashtuka sana kwani anapokutembalea usoni huona kuwepo kwa hali isiyokuwa ya kawaida,lakini wateja wetu huhisi raha ya ajabu pindi konokono wanapoendelea kutambaa kwenye nyuso zao kwa matibau”
Kusinga “massage”ya nyoka
Nyoka hufanya kazi ya kwanza ambayo itamlazimu mteja kulala chali na wao kupita juu ya mwili wake.Baadae hutembea mpaka shingoni na kusinga kwa mda kasha hushika mpaka kiunoni.
Kabla ya kuanza kazi nyoka hao hufungwa kwa mikanda maalumu mdomoni mwao,ili kuhsakikisha hawawezi kumdhuru mteja na hubandikwa plaste maalumu ili kutotoa hata tone la sumu ambayo inaweza kudhuru ngozi ya mteja.
Matibabu hayo ya dakika 90 hugharimu rupia 480,000 sawa na dola 43 ambapo  kwa fedha za Tanzania ni Shs 69,000
Nchini Indonesia kuna wateja wachache ambapo walio wengi hutokea bara la Ulaya,Jaspan au Korea Kusini .
Nyoka hao wanatunzwa katika nyumba moja iliyojengwa kwa kutumia mbapo katika kisiwa kimoja kilichopo bali,na wamekua wakilishwa chakula cha Sungura ili kuishi.
Hata hivyo haki za wanyama pamoja na watu wa haki za Binadamu wamekua na wasiwasi mkubwa kutokana tiba hiyo.Watu wa haki za wanyama wamezungumzia tiba hiyo kama “unyonyaji”
“Tunachukizwa kusikia kuhusu aina yoyote ya unyonyaji dhidi ya wanyama wakiwemo nyoka”alisema mmoja  wa wanaharakati hao wa haki za wanyama.
JE KWETU TANZANIA KWANINI NASI TUS IWE TUNA WATUMIA WANYAMA HAO KUTUINGIZIA KIPATO KAMA HICHO BADALA YA KUWAUZA NA KUWASAFIRISHA NCHI ZA NJE?

SOURCE OF INFORMATION  MWANANCHI 16 NOVEMBER 2013 PAGE 5

No comments:

Post a Comment