Social Icons

Sunday, 24 November 2013

JE WAJUA? HUYU NDIYE KIRUKANJIA WA TANZANIA


 Kirukanjia ni mnyama jamii ya wanyama wanaopatikana katika nchi za Djibout,Eritrea,Ethiopia,Kenya,Somalia,Sudan,Tanzania na Uganda.Kitaalamu Kirukanjia anajulikana kama Xerus rutilus.


Ni wanyama wanaopatikana katika maeneo ya kitropiki yenye vichaka vifupi vifupi, nyasi na katika maeneo ya miinuko yenye miamba.

Tanzania ni nchi mojawapo ambapo wanyama hawa wanapatikana.Chakula cha Kirukanjia ni mizizi,nafaka,matunda,wadudu,mayai ya ndege pamoja na wanyama wadogo sana.

Maadui wakubwa wa Kirukanjia ni binadamu kutokana na kuwindwa kwa ajili ya nyama kwa baadhi ya jamii lakini zaidi uharibifu wa makazi yao kutokana na uharibifu wa mazingira.

Uzazi wa Kirukanjia mara nyingi hauna muda maalumu.Hata hivyo,vichanga huonekana miezi ya Julai hadi Octoba katka mwaka.Mimba ya Kirukanjia huwa ni kwa siku 48 na vichanga hunyonyeshwa kwa siku 52.

Kirukanjia anaweza kuzaa mtoto mmoja hadi watatu.Jike hupevuka akiwa na umri wa miezi 10 wakati dume hupevuka akiwa na umri wa miezi minane tu.Japokua majike kuzaliana katika kipindi chote cha mwaka,lakini ni asilimia 10 tu ndiyo wanaweza kuzaa zaidi ya mtoto mmoja kwa mwaka.

Hali hii pia huweza kuwasaidia kupanga uzazi kiasili.Tofauti na wanyama wengine jamii ya mamalia wenye ushindani katika maeneo anayomilikiwa nao,maeneo yaliyo chini ya miliki ya kundi fulani la Kirukania huweza pia kutumiwa na kundi jngine.

Nijukumu la sisi Watanzania kuhifadhi makazi ya wanyamapori kwa kuwa ni suala la sisi sote.Wanyamapori hawa ni urithi wetu,kila mmoja wetu atimize wajibu wake kwa nafasi yake ili kuhakikisha uwo wa rasilimali ya wanyamapori na matumizi yake vinakuwa enendelevu.

No comments:

Post a Comment