Social Icons

Wednesday, 20 November 2013

MJUE FISIMAJIFisimaji ni familia pana yenye kubadilika ya wanyamapori walao nyama inayopatikana sehemu mbalimbali za Duniani ikiwemo Afrika 

Wataalam wa historia ya kisayansi wasema kundi la Fisimaji lilijitokeza yapata miaka milioni 40 iliyopita.

Zipo jamii mbalimbali za Fisimaji zenye tabia na ukubwa tofauti ambapo mdogo kabisa analingana na Panya wa kawaida na mkubwa ana uzito wa kilo 45.

Kwa lugha ya Kiingereza Fisimaji hutambulika kama Otter.Fisimaji pia wanasifika sana kwa uwezo wa kutumia mazingira mawili ya tofsuti msji kwa sjili ya mawindo na nchi kavu kwa ajili ya makazi,kuzaliana na kucheza.

Fisimaji ni wanyma wajanja, wenye uwezo wa kutumia nyenzo mbalimbali kwa ajili ya kutafuta chakula,kucheza na kujilinda.

Wanapotaka kula mayai makubwa ya Batamaji hulinyanyua juu kwa kutumia mikono yao yenye vidole vitano na kuligonga kwenye jiwe ili waweze kukifikia kiini chenye virutubisho mbalimbali

Chakula kikuu cha Fisimaji ni viumbe wa kwenye maji mfano Kaa,Samaki,Vyura,Minyoo na wadudu.

Fisimaji wana uwezo mkubwa wa kunusa mawindo yao kwakutumia manyoya marefu yaliopo kwenye midomo na pua kukusanya harufu za Samaki anaeogelea ndani ya maji au Kaa aliejiivha chini ya jiwe

Wakiwa kwenye maji Fsimaji wanapohisi hatari hujifica kwa kujiviringisha kama mpira pia hukaza misuli ya ngozi kiasi cha kuwashinda maadui wenye kucha au meno madogo kupenya.

Wakiwa nchi kavu Fisimaji hutembea polepole kuliko kwenye maji ambsko wana uwezo wa kuogelea kwa kasi wakitumia miguu kupiga kasi na mkiakuongeza na kurekebisha mwendo.

Fisimaji hupendelea kuishi kwenye eneo moja peke yake skitafuta chakula na kuendesha maisha yake mwenyewe kwa kumiliki eneo na kuweka mipaka kwa kutumia tezi zenye kutoa ute wenye harufu maalumu zilizopo karibu na tundu la haja kubwa.Fisimaji hutambua eneo la jirani yake na kulikwepa kwa kunusa tu.

Mipaka huvukwa wakati wa masika kwa sababu ya kujamiana kwa ajili ya kuzaliana ambapo dume humfuata jike na kukaa naye kwa muda mfupi mpaka mimba inapotungwa halafu hurudi kwake.

Baadhi ya jamii za Fisimaji zana uwezo wa kipekee kabisa miongoni mwa viumbe wote kwani iwapo hali siyo nzuri huweza kuhairisha kipindi chs kuzaa hadi mwaka mmoja tangu mimba ilipotungwa,kwa kuzuia ai lililorutubishwa na mbegu za dume kuingia kwenye mji wa uzazi hivyo kusimamisha ukuaji wke likiwa lanatunzwa vizuri ili kuendelea kuwa hai.

Fisimaji huzaa watoto wawili hadi watano baada ya kubeba mimba kwa miezi miwili na siku kadhaa ambapo watoto hukaa na mama yao kwa miezi kumi na mili na ndipo huachwa wanapoachwa wakatafute maisha yao wenyewe.


No comments:

Post a Comment