Social Icons

Thursday, 21 November 2013

PATA KUMJUA MNYAMA KURO NA MAISHA YAKEKuro ni mnyama aitwaye Kobus kwa lugha ya Kilatini lakini Kobus linalotokana na neno Koba.Koba lina asili ya kiafrika.Jina lake la kisayansi ni Kobus ellipsiprymnus defassa ambapo ellipsiprymnus humaanisha pete nyeupe.Kuro ni mnyama anayependelea kukaa jirani na mito,mabwawa kwa ajili ya kujikinga na adui zake.Hata hivyo mnyama huyu si mnyama anaeishi majini kama vile Mamba na Kiboko ila hukimbilia huko kwa ajili ya kujikinga tu na adui.

Kuro ni mnyama anayekula nyasi akiwa na ukubwa wa inchi 50.Mnyama huyu anapatikana katika uoto wa nyasinyasi maeneo ya savanna na maeneo ya mapori yenye miti miti.

Kuro dume huwa ni mkubwa kimaumbile kuliko Kuro jike,Kuro dume pekee yao ndio wana pembe zenye mikunjo kunjo na huwa na uzito wa kilogram 200 hadi 300 ,hupenda kukaa katika makundi ya hadi kufikia 300.Majike wana uzito wa kati ya Kilogram 160 hadi 200 na hupenda kukaa kwenye makundi yenye idadi ya hadi kufikia 600.

Kuro ni wanyama wenye uwezo wa kuona usiku na mchana na kwa kawaida huisha katika eneo la kilomita za mraba 1.2.Kuro huweza kuchukua mimba kwa muda wa siku 280 na huzaa ndama mmoja tu

Utalii hususani wa wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.

TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA MAZINGIRA.

No comments:

Post a Comment