Social Icons

Wednesday, 4 December 2013

LIFAHAMU ZIWA RUKWA AMBALO NDILO ZIWA KUBWA LA MAGADI NCHINI TANZANIA


Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa la magadi nchini Tanzania. Liko upande wa kusini magharibi ya nchi karibu na Zambia kati ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
Uenezaji wa ziwa hubadilika mara kwa mara kufuatana na idadi ya mvua inayonyesha katika beseni yake.

Ziwa liko kwa kimo cha mita 800 juu ya UB katika bonde ambalo ni mkono wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Bonde hili ni sehemu ya kusini ya mkono wa magharibi wa bonde hili na mikono yote miwili inaungana huko Mbeya kabla ya kuendelea kwa pamoja katika Ziwa Nyasa.

Beseni ya ziwa line eneo la takriban 80,000 km². Urefu na upana wake hubadilikabadilika kulingana na kiasi cha mvua inayonyesha. Kati ya mito inayoingia ni mto wa Songwe pekee ulio na maji muda wote. Kuna taarifa ya kwamba ziwa lilipotea wakati mwingine isipokuwa beseni ndogo upande wa kusini Songwe inapoingia hubaki na maji. Kama maji ni mengi ziwa lina urefu wa kilomita 180.

Eneo la ziwa ni kavu sana na maji yake ni ya magadi. Kwa hiyo hakuna vijiji mbali na mito hasa upande wa kusini. Majirani ni hasa Wafipa na Wasafwa.
Pamoja na maanzari mazuri Ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya linatarajiwa kila mwaka kufungwa kwa miezi sita kwa lengo la kutoa fursa kwa samaki kuzaliana na kukua.

Kwa mujibu wa uongozi wa Wilaya ya Chunya Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia kasi ya kutoweka kwa samaki katika ziwa hilo  ambapo hivi sasa wavuvi wanavua samaki wachanga mfano wa dagaa ambao hawafai kwa kitoweo.

Ziwa Rukwa tangu uhuru limetoa ajira katika sekta ya uvuvi ambapo wavuvi wameweza kusomesha watoto wao,kujipatia kipato kwa kuuza samaki na kupata kitoweo ambacho kinajenga afya kutokana na samaki wanaopatikana kwenye ziwa hilo.

Kutokana na uharibifu wa mazingira katika ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Chunya umesababisha mazalia muhimu ya samaki ndani ya ziwa hilo kuharibika kutokana na shughuli za kibinadamu zinazotokana na uingizaji wa mifugo mingi pamoja na uvuvi wa kutumia kokoro ambao umesababisha samaki wengi kutoweka na kubakia samaki wachanga pekee.

Ng'ombe wakiingizwa ndani ya ziwa Rukwa kwa ajili ya malisho na kunywa maji pia wanaharibu mazalia ya samaki ambayo yapo kwenye magugu yanayoota ndani ya ziwa hilo 

No comments:

Post a Comment