Social Icons

Sunday, 1 December 2013

MJUE MNYAMA NGIRI NA MAISHA YAKE
Ngiri ni Mnyamapori mtukutu huwasumbua wakulima wa mihogo na viazi vitamu hivyo hulazimika kuwindwa lakini huweza kukimbia kwa kasi kati ya kilometa 48 kwa saa kwa urefu wa  mita 200 mwendo ambao ni wa kasi zaidi kuliko wanariadha yeyote duniani.
Ngiri ana pua kubwa,macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi uliopinda au ulionyooka.Huwa  ana mwili mkubwa,miguu mifupi na nywele zilizojiviringisha.Ana kwato nne kwa kila mguu,mbili ni kubwa za mbele zikitumika kutembelea.
Ngiri huweza kuzaa msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropic,lakini hasa misimu ya mvua.Ngiri jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18 kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba.Ngiri dume huweza kushiriki maswala ya uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka 10.Kwa uzao mmoja,wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12waitwao vibwagala kasha kuachishwa kunyonya,familia mbili au tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana
Kitaalamu Ngiri wanaopatikana  hapa  nchini  wanaitwa Phacochoerus africanus massaicus ambao.
Ngiri wana umbo lenye manyoya machache na urefu wa mita 1.5,wanasimama kwa urefu wa kwenda juu kwa kati ya sentimita 63.5 na 85 hadi mabegani pia wanawastani wa uzito wa kilo 45 hadi 75 kwa majike na kilo 60 hadi 150 kwa madume.
Miguu ya Ngili ina mifupa migumu iliyounganishwa na misuli yenye  nguvu ambayo hufanya kazi ya kuchimba,kuruka na kukimbia kwa mlipuko kutokana na uwezo wa kukunjika na kunyooka haraka.
Ili kupata mwendo kasi wa juu Ngili hunyoosha kichwa mbele na mkia juu ili kuweza kuuweka mwili sawa na kuimarisha mwendo asianguke.
Ngiri hawana tezi za jasho hivyo hujipoza kwa kutumia maji au matope wakati wa joto kali.Pia hutumia matope  kama njia ya kujikinga na kuunguzwa na jua.Zaidi matope huzuia wasiathiriwe na inzi na wadudu.


Utalii hususani wa wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.

No comments:

Post a Comment