Social Icons

Wednesday, 15 January 2014

HUU NDIO MSITU MKUBWA WA MITI ULIOPO SAO HILL IRINGA TANZANIA

Tumekuwa tukisikia sana kuhusu pori kubwa na lenye miti mingi kulipo yote tanzania ambayo ni ya kupandwa, lakini hatujapata nafasi ya kuliona. Pori hilo kubwa lipo Barabara ya kimataifa inayotokea Dar es salaam  Kuelekea Zambia ni Msitu wa Sao Hill uliopo Iringa Tanzania. Msitu huu una miti ya kupandwa kwa ajili ya kutengenezea karatasi na matumizi ya mbao.Tazama hapa chini muonekano wa msitu huo.
 Hii ni sehemu ya kuingilia katika msitu huo ukitokea mkoani Mbeya 
 Ukungu huu mkubwa unatokana na hali ya hewa 

Unaweza ukasema mbele hapapitiki lakini ni hali halisi ya ukungu mkubwa 
 Hii ni miti kama inavyo onekana, imepandwa kwa umahili wa hali ya juu
 Ndani ya msitu huo wwenye Kilometa zaidi ya 10, Magari hupita bila wasiwasi kwa sababu ni eneo lililo salama 
 Hata watembea kwa miguu wanapita katika msitu huo 
 Hili ni eneo la wazi kiasi katika msitu huo 
Picha zote na Maliasili zetu Blog

No comments:

Post a Comment