Social Icons

Tuesday, 7 January 2014

MATOKEO YA SENSA YA TEMBO NCHINI KUTANGAZWA JANUARY 10 JIJINI DAR ES SALAAM


 Pichani  ni  kundi la Tembo  wakiwa katika hifadhi ya Ruaha Iringa kama  walivyonaswa na kamera ya matukiodaima.com 
............................................
Tafadhali husika na kichwa tajwa hapo juu. Mhe. Naibu Waziri, Lazaro Nyalandu atakutana na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini na wadau mbalimbali wa sekta ya Maliasili na Utalii kutangaza rasmi matokeo ya sense ya tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana katika mifumo ikolojia ya Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa.

Wizara inatoa mwaliko kwa waandishi wote kuhudhulia mkutano huo utafanyika Ijumaa ya Tarehe 10/01/2014 saa 4:00 asubuhi katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Imetolewa na Chikambi K. Rumisha Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii 7/1/2014

No comments:

Post a Comment