Social Icons

Sunday, 26 January 2014

TANAPA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU ILIWAWEZE KUPAMBANA NA UJANGILI‏


Na  Walter Mguluchuma-wa Katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi  za  Taifa  za Wanyama pori   TANAPA   Allani  Kijazi  amewataka  Askari  wa Hifadhi za Taifa  za Wanyamapori  kufanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa  ilikuweza  kupambana  na mitandao ya Ujangili  iliyopo hapa Nchini  na  nje ya nchi   na kulinda  maliasili zilizopo
Kauli hiyoaliitowa hapo  juzi  wakati akifunga  mafunzo  ya awali ya miezi mitatu  ya Askari  wa Hifadhi  za Taifa za Wanyama pori  katika chuo  cha Mlele  kilichopo  Wilayani Mlele Mkao  wa Katavi  ambapo jumla ya Askari 96 wa TANAPA walihitimu  mafunzo hayo  kati yao akiwepo  mwanamke mmoja
Kijazi  alieleza kuwa  Nchi yetu imekubwa na wimbi kubwa  la ujangili  hivyo ni vizuri  katika kupambana   na vita hiyo ya ujangili  Askari  wakafanya kazi zao  kwa uadilifu mkubwa  na kwauaminifu
Alisema kila Askari  wa TANAPA atambue kuwa  anawajibu  wa kupambana  na kutokomeza  ujangili  na kulinda  na kusimamia Rasilimali  za nchi  yetu  na wanatakiwa  kuwa  na uzalendo
Aliwaeleza wahitimu hao  kuwa  Shirika la Hifadhi la Taifa la wanyama pori TANAPA  limejipanga  na litahakikisha  linakabiliana   na   ujangili wote uliopo  hapa Nchini 
Alifafanua kuwa shirika  linaandaa utaratibu wa kubadilisha mfumo wake  ilishughuli  zake  ziweze kubadilishwa kutoka  kwenye kirai  na kuwa  kwenye mfumo wa  kiaskari  ambao utakuza  nidhamu
Alisema wapo  baadhi ya watumishi wa TANAPA wamekuwa wakitowa siri za shirika  na watakao bainika   atahakikisha  wanachukuliwa hatua za kinidhamu  kama vile kufukuzwa kazi  kwani TANAPA haita  wavumilia watu wa  wenye tabia hito au mtu mwenye tabia hiyo
Kwa upande wake Mkurugemzi  wa  utumishi  na utawala  wa TANAPA Witnes  Shoo aliwaka Askari wa Hifadhi  za Taifa  za wanyama kufanya kazi zao kwa kuzingatia viopo vyao
Pia aliwataka waliwataka Askari kutojishughulisha  na  maswala yoyote  ya ujangili  kwani kufanya hivyo  ni kinyume  cha sheria  za   N chi
Katika risala yao ya wahitimu   wa mafunzo hayo ya awali ilyosomwa na Bruno  Mbunda  walieleza kuwa mafunzo  hayo walioyapa  

No comments:

Post a Comment