Social Icons

Friday, 3 January 2014

Wafugaji wapatiwa mizinga ya nyuki yenye thamani ya Milioni `17 za KitanzaniaNa Walter Mguluchuma-Mpanda Katavi.
Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali UDESO imetengeneza mizinga 270 yenye thamani ya shilingi milioni 17 kwa ajili ya kuvipatia vikundi saba vya wafugaji wa nyuki katika Wilaya ya Mlele Mkoani katavi.

Hayo yamesemwa hapo jana na Mkurugenzi wa Taasisi  ya Usevya Development Society (UDESO) Eden Wanyimba wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katavi.

Alisema Taasisi hiyo ambayo inajishughulisha na masuala ya Mazingira imeamua  msaada huo wa mizinga ya kisasa kwa wafugaji wa nyumi ili kuwawezesha wafugaji kuongeza uzalishaji wa asali iliyo bora tofauti na hapo awali .

Alifafanua kuwa uzalishaji kwa wafugaji wa nyuki utaongezeka toafuti na hapo awali kwa kuwa mizinga hiyo ya kisasa ina uwezo wa kuzalisha lita 20 kwa kwa wakati mmoja tofauti na hapo awali,walipokuwa wakitumia mizinga ya kienyeji inayozalisha lita nane kwa msimu.

Endapo watatumia vizuri mizinga hiyo watanufaika kutokana na asali yake kuwa bora nainasoko kubwa hivyo hali ya uchumi kwa wafugaji wa asali itaongezeka.

Pia (DESO) imenunua Pikipiki mbili zenye thamani ya shilingi milioni 6.8 kwa ajili ya kuzipatia msaada  Halmashauri za Wilaya ya Mlele na Nsimbo,kwa lengo la kuwawezesha maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi  wa Jamii kurahisisha utendaji kazi zao.

Chanzo: Katavi yetu blog

No comments:

Post a Comment