Social Icons

Tuesday, 18 February 2014

JESHI LA POLISI LAKAMATA MENO YA NDOVU YENYE THAMANI SHILINGI MILIONI 17 SINGIDA‏Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP.Cordula Lyimo, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo juu ya kukamtwa kwa meno ya Tembo vipande 16 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 17 milioni.Vipande hivyo vimekamatwa februari 16 mwaka huu saa tano usiku kwenye kizuizi cha mazao cha kijiji cha Ukimbu wilaya ya Manyoni. Siku nne zilizopita,vipande vingine 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi 43 milioni,vilikamatwa eneo hilo hilo.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata vipande 16 vya meno ya ndovu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17.
Meno hayo yamekamatwa siku nne (12/2/2014) toka meno mengine vipande 21 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 43 milioni, kukamatwa kwenye eneo lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha Ukimbu kata ya Mgandu wilaya ya Manyoni.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Singida.SSP.Cordula Lyimo amesema meno hayo yamekamatwa febr.16 saa tano usiku huko katika kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha Ukimbu,kata ya Mgandu tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni.
Amesema askari wakiwa katika kizuizi hicho,walifanya ukaguzi kwenye gari T.288 AJF aina ya scania mali ya kampuni ya super service likiendeshwa na dereva Ally Hamadi, likitokea Makogorosi Chunya,likielekea Itigi wilaya ya Manyoni.
“Baada ya upekuzi huo,walikuta meno hayo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya begi la nguo na kuwekwa kwenye keria za ndani ya basi.Mtuhumiwa aliweza kupatikana wakati akiwa katika juhudi za kutaka kutoka nda ya basi ili akimbie”,amesema Lyimo.
Kaimu kamanda huyo,amesema uchuguzi zaidi unaendelea ili kubaini au kupata mtandao kamili unaojihusisha na kuwinda pamoja na kununua nyara hizo.

No comments:

Post a Comment