Social Icons

Monday, 17 February 2014

Meno ya tembo ya mil. 700/- yakamatwa Mtwara


Wakazi watatu wa Dar- es- Saalaam wamekamatwa na polisi mkoani Mtwara wakiwa na vipande 58 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 700. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa  Maisha Manganga, alisema watuhumiwa hao ni Hamid  Abdallah Ngunde (40),  Geraldat Mmuni (36)  na Boniface  Msogo (29). Baada ya kukata chini ya kiti cha abiria cha  nyuma ya dereva  na kutengeneza tangi bandia na kuyaficha meno hayo.

Alieleza kuwa 'majangili hao' walikamatwa juzi saa 11 alfajiri katika kijiji cha Chungu mkoani hapo na kufafanua kuwa walikuwa na vipande 58 vyenye kilo 130.6.
Kwa mujibu wa Maganga, watuhumiwa hao walikamatwa katika kizuizi cha barabara ya Mtwambaswala-Mangaka wakiwa kwenye Land Cruiser  namba   T  208 AGC mali ya Hilali Rashid mkazi wa Dar-es-Salaam.
Akizungumza na wanahabari alisema walikata sakafu ya gari kwa chini na kutengeneza tangi hilo   bandia na wakatandika zulia juu yake.
Walibomoa chini ya  kiti cha abiria kilicho nyuma ya dereva. "Alisema Maganga.
Alifafanua kuwa, watuhumiwa kwa pamoja  wanashikiliwa na  kwamba watafikishwa mahakamani baada ya  uchunguzi wa awali kukamilika.
Hatua hii inakuja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzungumza kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC alisema serikali imebaini mtandao unaojumuisha watu 40, akiwemo tajiri maarufu mkoani Arusha.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment