Social Icons

Wednesday, 12 March 2014

TAARIFA KWA UMMA:UZINDUZI WA SIKU YA TAIFA YA KUTUNDIKA MIZINGAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
UZINDUZI WA SIKU YA TAIFA YA KUTUNDIKA MIZINGA
TAREHE 18 MACHI 2014
Siku ya Taifa ya Kutundika Mizinga itaadhimishwa kitaifa mkoani Katavi katika wilayani Mlele tarehe 18 Machi 2014. Aidha, siku hiyo mikoa mingine itaadhimisha kimkoa katika wilaya na vijiji vilivyochaguliwa.  Kauli Mbiu ya mwaka huu ni: “Boresha Ufugaji Nyuki, Linda Ubora wa Mazao Yake”.

Madhumini ya siku hii ni kuendeleza Ufugaji Nyuki unaolenga kuongeza idadi ya wafuga nyuki, usimamizi bora wa makundi ya nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuzingatia ubora na teknolojia za kisasa. Aidha, siku hii inatumika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa raslimali za misitu na nyuki.

Siku hii itakuwa chachu ya kuwahamasisha wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kwa wingi katika ufugaji nyuki wa kisasa. Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), ambaye atashiriki kutundika mizinga katika msitu wa Mlele Kusini eneo la Kanembela na baadaye kuhutubia wananchi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kufanikisha siku hii kwenye maeneo yaliyopangwa na maeneo binafsi.
MAENEO YATAKAYOTUNDIKWA MIZINGA KATIKA MIKOA MBALIMBALI TANZANIA BARA
NA
MKOA
WILAYA
KIJIJI
MHUSIKA/
WAHUSIKA
ENEO LA KUFUGIA
1
Simiyu
Busega
Mkula
Kikundi cha Imarika
Msitu wa Kikundi na Kijiji
2
Geita
Geita
Itina
Kikundi cha Itina
Msitu wa Kijiji (Ngitiri)
3
Mwanza
Ilemela
Kasamwa
Kikundi
Ngitiri ya kijiji
4
Mara
Musoma
Magereza
Msitu wa Magereza
5
Kagera
Missenyi
Kenyana
Kikundi cha Shubira
Miti katika Mashamba
6
Ruvuma
Songea
Mtyangimbole
Kamati ya Usimamizi Shirikishi Misitu
Misitu wa Songea Fuel
7
Mtwara
Mtwara
Mnivata
Kikundia
Msitu wa Halmashauri Mtiniko Mnivata
8
Lindi
Ruangwa
Liuguru
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
Msitu wa Kijiji Liuguru
9
Iringa
Iringa
Mgera na Mngalali
Msitu wa Ubena
Mufundi
Shamba la Miti Sao Hill
Shamba la Miti Sao Hill
Shamba la Miti Sao Hill
10
Mbeya
Momba
Chilanu na Nzoka
Vikundi vya Ufugaji Nyuki
Mlima Malinde
11
Njombe
Ludewa
Mapogoro na Mavale
Vikundi vya Ufugaji nyuki
Msitu wa Sikaranyumbo
12
Rukwa
Kalambo
Kisumba, Kafukoka
Vikundi vya ufugaji nyuki
Msitu wa mto Kalambo
Nkasi
Vijiji (5) Chala A, B, na C, Chalakima na Chatekelesha
Vikundi vya ufugaji nyuki kila kijiji mizinga 10
Msitu wa Mlima Chale
13
Tanga
Korogwe
Mkwakwani Myusi
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
Hifadhi ya asili Amani
14
Arusha
Arumeru
Nkwenankoli
Kamati ya Maliasili ya Kijiji
Hifadhi ya Msitu wa TFS
15
Kilimanjaro
Moshi
Kahe
NGO
Msitu wa Halmashauri
16
Tabora
Sikonge
Utyatya
Kikundi cha Wafugaji Nyuki Nyahua
Bwawa la Utyatya
17
Kigoma
Uvinza
Uvinza
Kazaroho beekeepers cooperative society
Msitu wa Basanza
18
Shinyanga
Shinyanga
 Ukimbagu
NAFRAC na Kikundi cha Wafugaji Nyuki Ugimbagu
Shamba la Albano Malila
19
Katavi
Mlele
Kanembela
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
Msitu wa Mlele
20
Morogoro
Ulanga
Mselezi
Kikundi cha ufugaji Nyuki SEMA
Msitu wa Hifadhi Mselezi
Gairo
Msingisi
TFS – Meneja Wilaya
Msitu wa Hifadhi Msingisi
21
Pwani
Bagamoyo
Msinune
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
Msitu wa Simbo
Mkuranga
Kibuyuni
Kamati ya Maliasili na Mazingira ya kijii
Msitu Masanganya
22
Dodoma
Kongwa
Nyamkonga
Kikundi cha Ufugaji Nyuki
Msitu wa Halmashauri ya Wilaya
23
Singida
Mkalama
Nkungi
Kikundi cha ufugaji Nyuki
Msitu wa Kijiji
24
Manyara
Babati
Haraa
Kikundi cha ufugaji Nyuki
Msitu wa Kijiji
Imetolewa na:
S.Gesimba
Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Maliasili na Utalii,
11/03/2014

No comments:

Post a Comment