Social Icons

Friday, 4 April 2014

TUKIO LETU LA WIKI: MTAZAME PAKA HUYU ALIYE WATUNISHIA MISURI SIMBA WA NNE!


 Paka huyu aliingia katika Himaya ya Simba Wa nne na kupambana nao vikali ingawa mwisho wa siku aliishia kutwangwa vilivyo..

Paka huyo mdogo baada ya kuingia katika himaya hiyo ya wababe hao wa mwituni alianza kuleta vurugu kwa kutumia meno na kucha zake huku akitishia kupambana na Simba hao

Baada ya Mkwara wa muda mrefu Simba waliamua kumng'ata ng'ata na kumuua

Hivi ndivyo ilivyokuwa....
Hapa paka huyu akiwa analia huku akimtishia Simba ...
Simba hawa wa nne wakionekana Kumshangaa Paka ambaye alikuwa akiwatishia 
Simba walipochoka na Kelele zake wakaamua kuanza kumfanyizia 
Hapa paka akiwa hoi baada ya kuburuzwa vilivyo na Simba


Mmoja wa Simba akiwa amebeba Mzoga wa Paka huyo Baada ya kuuawa

No comments:

Post a Comment