Social Icons

Saturday, 7 June 2014

HATARI: SIMBA ALA NG'OMBE KUMI NA MOJA NA MBUZI WA NNE!

Na  Walter Mguluchuma
Jumla ya Ng’ombe  kumi  na Moja  na mbuzi wanne wameuwa  na kuliwa na  mnyama simba   katika   matukio  matatutofauti   yaliyotokea    katika  Tarafa ya  Nsimbo Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi  baada ya simba kuvamia katika vijiji vitatu  
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Mtapenda Elieza Fyula  tukio la kwanza  lilitokea  hapo  Mei  28  majira ya usiku  katika Kijiji  cha Kabatini
Katika tukio hilo  Simba  wa  walivamia  kwenye kijiji  hicho na kuuwa na kula  Ng’ombe  watatu  na mbuzi  watano  ambao walikuwa  wako ndani ya zizi la  kufugia mifugo
Alisema  siku  iliyofuata ya tarehe 29 meimajira ya usiku  simba hao  walivamia  katika  Kitongoji   cha Kambike   kilichoko  katika  Kijiji cha Isinde  na  kuwauwa Ng’ombe  watano  mali ya  mfugaji wa kitongoji hicho aitwaye  Dirisha  na kisha  waliwala ng’ombe hao
DiwaniFyula  alieleza  baada  ya tukio hilo  viongozi wa kitongoji  walitoa taarifa kwa viongozi wa kata ambao  waliwasiliana na Idara ya Wanyama Poli ambao waliwasili kijijini hapo na kuwaswaga simba hao wapatao watano
Alisema siku iliyofuata simba hao walivamia tena kwenye kijiiji cha mkumbi  na kisha waliuwa Ng’ombe wawili na kuwala  
Na Blogs za mikoa 

No comments:

Post a Comment