Social Icons

Friday, 13 June 2014

VIPANDE 26 MENO YATEMBO VYANASWA DAR


KAMISHINA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na vipande 26 vya meno ya tembo kinyume cha sheria.

Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kova alisema, tukio hilo lilitokea Mei 29 mwaka huu maeneo ya Mwananyamala Kata ya Mwinyijuma Osterbay jijini Dar es Salaam.

Alisema, baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtu ambaye jina lake limehifadhiwa kuwa, kuna gari lenye namba za usajili T 178 BSY aina ya Noah ambalo wanalitilia hofu kutokana na mzigo uliokuwepo ndani, walijipanga na kuweka mtego.

Alisema, baada ya kuweka mtego huo waliweza kufanikiwa kulikamata gari tajwa na walipopekuwa walikuta viroba viwili vilivyokuwa na vipande 26 vya meno ya tembo ambavyo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.

Aidha, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Adam Oyona (37)mkazi wa Mbagala, Selemani Leonard (37) mkazi wa Mwananyamala na Hussein Said (34).

Aliongeza kuwa, Juni 5 mwaka huu Polisi wa Wilaya ya Buguruni kwa kushirikiana na Mhifadhi wa Wanyamapori Makao Makuu, Bakari Yusuph (33) mkazi wa Mbezi Beach walifanikiwa kukamata vipande 28 vya meno ya tembo vyenye thamani ya sh. milioni 275,550,000 nyumbani kwa Dominick Kolineli (35) mkazi wa Tabata Kisukuru.

Alisema, baada ya kufanya upekuzi katika nyumba hiyo kwenye chumba cha uani cha Herbert Machaka (30) mkazi wa Morogoro kilipatikana kipande kimoja cha jino la tembo.

“Upekuzi uliendelea katika stoo na jiko ambako walipata vipande 27 vya meno ya tembo na kuweza kufikia idadi ya meno ya tembo 28,”alisema Kova.

Alisema, watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa ujangili huu unaomaliza rasilimali za Taifa.

Chanzo;Majira

No comments:

Post a Comment