Social Icons

Monday, 30 June 2014

Yafahamu mataifa ya Afrika yanayotumia wanyama na ndege kama nembo ya taifa (Wanyama wa Taifa)‏

TANZANIA
Nchi ya Tanzania inatumia mnyama Twiga kama alama ya taifa/nembo na kwa hiyo analindwa na sheria. 

image.jpeg

Ingawa tangazo la kipekee huweza kutolewa na Rais, huwa kawaida, kuua Twiga kunaweza kukusababisha kufungwa jela. Twiga ni mnyama mpole mwenye shingo ndefu inayowakilisha uwezo wa kuona mbali tukiwa bado tunaangalia yaliyopita na ya sasa. Twiga pia anawakumbusha Watanzania kutumia nguvu zao na kuwa tayari kujipanga kimwili, kiakili na kiroho kama twiga.

Angola
Nchi ya Angola ina mnyama wa taifa na ndege wa taifa, huitwa Magnificent Frigatebird na swala. Ndege huyu ameitwa hivi kutokana na hadithi ya usawa ya - the Man O'War. 
Ameitwa hivyo kutokana na ukimya wakati wa kuruka, kasi na tabia yake ya kuiba nyama kutoka mwa ndege wengine. Swala mweusi nchini Angola wako katika hatari.
Lesotho
Mnyama wa taifa wa nchi ya Lesotho ni faru mweusi. Makazi hatari kwa mnyama huyu yalikuwa ni mashariki na katikati mwa Africa. Faru sasa wana maisha magumu nchini Afrika Kusini kutokana na uhitaji wa pembe zao kwa madai ya dawa za asili ya kichina. 
Hivi karibuni raia mmoja wa kigeni amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kosa la uwindaji haramu wa faru. Faru anachukuliwa kuwa na kinga ya asili kutokana na ngozi yao nyembamba, ukubwa na pembe – kuwafnya kuwa alama ya taifa.
Madagascar
Mnyama wa taifa la Madagascar ni komba bukini, mbegu ya pekee ambayo inapatikana katika kisiwa hicho cha barani Africa pekee. Komba bukini wanaaminika kuwa wamekuwepo kisiwani hapo kwa miaka 65 million iliyopita. 
Wanyama hawa wapo katika hatari ya kutoweka kutokana na tabia ya uwindani na usafirishaji. Komba bukini hutumiwa sana na watu wanaosoma nadharia ya mabadiliko kutokana na upekee wake.
Nigeria na Ghana
Tai ni chaguo lingine maarufu, kwa nchi kadhaa kuchagua tai au tofauti yake kuwa mnyama wa taifa. Hii inajumuisha nchi za Misri na Mauritius hutumia tai wa rangi ya dhahabu, Nigeria na Ghana tai na nchi za Sudan Kusini na Zambia hutumia tai-samaki wa kiafrika. 
Tai hujulikana kutokana na kasi yao na size, na nafasi yao ya uwindaji katika ulimwengu wa ndege, hii huwafanya kutumika kama alama ya taifa. Tai wa kike katika vizazi vyote huwa wakubwa zaidi kuliko tai wa kiume. Ni alama ya taifa katika mataifa mengi kama vile Marekani, Ujerumani, Albania, Hispania na mengineyo mengi.
Rwanda
Mnyama wa taifa la Rwanda ni cdhui wa kiafrika. Chui huyu wa kiafrika anajulikana kutokana na vidoti (mara nyingi hukosewa na kuitwa madoa). Pia upo uwepo wa chui weusi. 
Hupenda kuishi katika maeneo ya milimani, misitu mikubwa ya mvua na sehemu ya jangwa na hupenda kula chakula kingi pale wanapokipata. Wako katika hatari ya kutoweka kutokana na ushindani na binadamu juu ya makazi na majangili na huwa wakiwindwa.
Ivory Coast
Nchi ya Ivory Coast (sanjari na nchi za Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini) wamechagua tembo wa kiafrika kuwa mnyama wa taifa. 
Tembo wa kiafrika ni mnyama mkubwa zaidi miongoni mwa wanyama duniani. Wanachukuliwa kuwa miongoni mwa wanyama wenye akili ulimwenguni.
DRC
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina aina ya pekee ya mnyama wa taifa ajulikanaye kama okapi. Wanyama hawa wadogo wanaonekana kufanana na twiga (mnyama anayeonekana kufanana naye sana) na pundamilia (kutokana na marakaraka). 
Okapi wana ndimi ndefu za rangi ya bluu, ndimi hizi ni ndefu na huzitumia kuangalia masikio yao. Wanyama hawa hawapo katika hatari yoyote, ingawa, wanahitaji sehemu kubwa ya kususurika/kuzurura na sasa wanatishiwa kuwindwa na kuharibiwa kwa makazi yao.
Ethiopia na Liberia
Simba ni chaguo katika mataifa haya kuwa mnyama wa taifa tofauti na tai mkubwa. Simba ni mnyama mkubwa anayeishi katika jamii yap aka baada ya tiger, wana upeo na ni muwindaji mzuri katika maeneo yao ya asili. Wanaweza kupatikana katika maeneo ya jangwa la sahara barani Africa na bara la Asia. 
Simba inasemekana kuwa adimu huku ikisemwa kuwa, namba yao inapungua katika maeneo ya mashariki na kusini mwa kwa 30-50% katika kipindi cha miaka 20 iliyopita kutokana na kuiliwa makazi yao na binadamu. Vizazi kadhaa vya simba vimekuwepo tangu zamani sana. Nchi nyingine ambazo humtumia simba kama alama ya taifa ni Ubelgiji, Luxemborg, Uholanzi, Singapore na nyinginezo.
Botswana
Mnyama wa taifa la Botswana ni pundamilia, marakaraka ya farasi. Pundamilia hutofautiana kwa sababu ya marakaraka yao na sababu kwamba hawakuwahi kufugwa.
Kuna nadharia kadhaa zinazoeleza ni kwa nini pundamilia wana rangi ya namna hiyo.wanapatikana zaidi katika maeneo ya mashariki na kusini mwa Africa.
Algeria
Taifa lililopo kaskazini mwa Africa Algeria limemchagua mnyama mbweha kuwa alama ya taifa. 
Mbweha wanaotumika kama alama ya kitaifa ya Algeria ni wadogo sana kulinganisha na mbweha wengine duniani na huweza kutambulik kutokana na masikio yake makubwa.

No comments:

Post a Comment