Social Icons

Sunday, 20 July 2014

WAZIRI LAZARO NYALANDU AKUTANA NA BALOZI WA HESHIMA WA UTALII BEVERLEY, LOS ANGELES


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa (kushoto) na Bw. Abdul Majid baada ya kupokea taarifa ya mikakati wanayoitumia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kwa wamarekani jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiagana na Balozi wa Tanzania wa Heshima wa Utalii nchini Marekani Bw. Ahmed Issa mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala kadhaa ya kuvutia Watalii wa Marekani nchini Tanzania jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akizungumza na  Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa juu ya mikakati mbalimbali ya kuvutia watalii wa kimarekani kutembelea Tanzania jana Beverly, Los Angeles.

Mikakati inayotumiwa na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania Bw. Ahmed Issa kutangaza utalii ni pamoja na matumizi ya magari yenye picha za vivutio vya utalii wa Tanzania katika majiji mbalimbali katika California - Marekani kama inavyoonekana katika picha

No comments:

Post a Comment