Social Icons

Wednesday, 27 August 2014

MALIASILI ZETU WATEMBELEA ENEO LA KIJUNGU RUNGWE TUKUYU NA KUJIONEA MENGI

Yawezekana kabisa ya kuwa wewe ni mtanzania mwenzetu lakini kwa njia moja au nyengine umekuwa bize ukiangalia vivutio vya utalii, na mambo kama hayo katika DVD au Runinga yako Utalii wa nje na kusahau kabisa ama kwa kuto kufahamu juu ya Vivutio vizuri vya kitalii ambavyo vinapatikana Tanzania. 

Maliasili zetu Blog pendwa ambayo imejikita hasa katika maswala ya kitalii imeonelea ni vema ikaanza kuwaonesha mambo mbalimbali ambayo hujayafahamu lakini kwa kuanzia kwanza Tumefika moja kwa moja eneo Moja linaitwa Kijungu lililopo eneo la Rungwe Tukuyu.

Tuanze Safari yetu....
Kwanza baada ya kufika hapa Maliasili zetu ilishikwa na Butwaa kuona kiingilio kikubwa cha Tsh 5,000 kwa kichwa ambapo haijalishi mkubwa wala mtoto, na zaidi ni kwamba kiasi hicho analipia mzawa wa Tanzania, na wageni pia . swala hili lilitupelekea tuwaulize wahusika na wao kushindwa kutoa majibu yanayoridhisha. Baada ya utafiti tukagundua kuwa wanakijiji ndio wameweka hicho kibao kwa maslahi yao binafsi ili mgeni anapokuja achajiwe mara moja. kutokana na swala hili na hili eneo la Kijungu ni Muhimu Tungeomba kabisa Serikali iliangalie hili swala kwa ukaribu kabisa ili mambo yaende vizuri. na watu wengi zaidi waje tembelea hapa.
Hapa ni eneo ambalo Maji ya mto huo yanatokea katika eneo linaitwa Namba One eneo la ukanda wa juu kabisa wa eneo hilo, Majihayo pamoja na mengine mengi hata wakati wa mvua kubwa ni lazima yazunguke yanapo kwenda lakini mwisho wa siku ni lazima yaishie hapa, Pia hapa ndipo maji haya yanapoanza kutililikia moja kwa moja katika kijungu.
Maji hayo sasa huingia katika eneo hili la kijungu, Wamekiita jina la kijungi kwa sababu kubwa kuwa eneo hilo lipo kama chungu, Maji hayo hata yakiwa na kasi kiasi gani, hata yawe mengi kwa namna gani hayawezi kujaa katika Kijungu hiki, Pia kijungu hiki hakuna mtu aliyekijenga bali ni maajabu tuu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hilin eneo limeumbwa kwa miamba ya mawe yanayofanana na Chuma kigumu. Maji haya yakishafika hapa huwa si mwisho kuna eneo yanaelekea..kwa hakika ni maajabu na kama huna wazo la kutembelea ni wakati wako sasa.
Kulia ni upinde unao onekana kutokana na kasi ya maji, upinde huu ni kivutio kikubwa hasa wakati wa jua kali huonekana vizuri

Baada ya maji hayo yenye kasi ya ajabu kuingia katika kijungu hicho hutokea katika eneo hili ambapo yanaonekana meupe na yenye mapovu . hii ni kutokana na sababu ya kwamba yanakuja kwa kasi na kufikia hapa, baada ya kufika hapa mbele kunaonekana kwamba kuna  uwazi, uwazi huu kwa mujibu wa wanakijiji wanaotokea eneo hili wanasema kwamba maji haya huingia hapa katika uwazi ambao unakadiliwa kuwa  na urefu kwa Kilometa moja husafiri huko na baadae hutokea katika upande mwengine ambapo ukitazama vizuri katika picha hiyo kwa mbele ya haya maji kuna maji yamepoa hayana kasi hapo ndipo yanapo tokea, hakuna yanapo kutana haya maji mpaka yaingie pangoni ndio yatokee upande wa pili, hii itaonekana katika picha inayofuatia, hili ni moja ya ajabu kwa sababu waweza dhania haya maji yanakutana kumbe hayakutani hata kidogo.
Picha hii inaonesha vizuri na ni mwendelezo ya wa maelezo ya maji hayo hapa kama inavyo onekana upande wa juu ni kijungu maji ambapo yanaingilia hapo kisha yanatokea upande huo wa pili yanapoonekana meupe sana na povu kutokana na povu kisha yanaingia katika pango hilo linalokadiliwa kuwa na Kilometa moja kisha yanatokea upande wa pili hapo yanapo onekana kama yamepoa kisha kuendelea na safari , Cha ajabu maji hayo hayakutani hata kidogo.
Wa Kwanza kutoka kulia ni Fredy Njeje wa Maliasili zetu akiwa na Mzee Eliya Kabaghasya mzawa wa eneo hili
Tulipo wasili katika eneo hilo la kijungu tulipata wasaa wa kuongea na Mzee mmoja wa zamani sana ambaye kwa hakika yeye alikiona kijungu zamani sana miaka yani miaka ya 1933 , mzee huyo ambaye anatambulika kwa jina la Elia Kabadhasya aliye  zaliwa mwaka 1927 alieleza kwamba alikijua kijungu hiki wakati alipokuwa akitafuta sehemu ya Kunyweshea Ng'ombe Maji ndipo aliposhuka eneo hili na kukiona Kijungu hiki, hata hivyo wakati anawanywesha maji Ng'ombe wake kwa bahati mbaya moja kati Ng'ombe hao alitumbukia ndani ya kijungu hicho na kupotea moja kwa moja.  Kwanza kutoka kulia ni Fredy Anthony Njeje kutoka blog ya  Maliasili zetu akiwa anachukua maelezo kwa makini ya Mzee Elia Kabaghasya wa kati kati.  Mzee Eliya alieleza kwamba hili ni eneo zuri sana la utalii ambapo aliwataka watu wengi zaidi waje kutembelea katika eneo hili na kujionea mambo mengi zaidi na Maajabu ya Mungu ya eneo hilo la kipekee ambalo kwa Tanzania hata kwa Dunia ni hapo tuu ndipo papo hivyo, Alieleza zaidi kwamba maji hayo ya mto huo hutumika zaidi kwa ajili ya kunyweshea mifugo, na kufulia tuu hayatumiki kwa kazi zengine. Alitoa wito kuwa watu wanatakiwa kuwa makini wanapokuja kutembelea eneo hilo na kuchukua tahadhali kama maeneo mengine kwa kuwa mtu anaweza teleza ingawa eneo hilo kuna wataalam na watu maalum wa kuwaongoza. alimalizia kwa kusema kuwa kuna haja ya Serikali kukiboresha Kivutio hiki cha Kijungu.
 Mmoja wa wanakijiji ambao wanaishi katika eneo hilo akipita njia kati kati ya Kijungu hicho na kusema  kwamba zamani kutokana na imani za mababu zetu ilikuwa ili upite ni lazima utumbukize kitu chini ndio upate kupita hapo, lakini kadili siku zinavyozidi kwenda na hivi miaka ya karibuni imani hiyo imetoweka na mtu anaweza kupita bila shida, pia alisema kwamba katika eneo hilo mtu anapokatiza katika mwamba huo katikati anatakiwa aanze kutanguliza mguu wa kulia kwanza ndio anaweza akavuka. Mwisho alisema kwamba ukivuka upande wa pili unatokea moja kwa moja mpaka Uporoto ingawa ni parefu hivyo mababu zetu ndio njia walikuwa wakipita enzi hizo.
******
Inawezekana umehamasika na unataka na wewe kufika katika eneo la Kijungu kujionea wewe mwenyewe kwa macho yako na haya ndio maelekezo.

Namna ya kufika
Kutoka Mbeya Mjini hadi Sehemu moja inaitwa KK Wilaya ya Rungwe-Tukuyu ni zaidi ya Kilometa 50 , Baada ya hapo kuna njia ambayo inakatiza upande wa kulia kuelekea Chuo cha Magereza, Ukifika Chuo cha Magereza ndani utapata maelekezo yote ya namna utakavyofika, Muhimu kufuata taratibu maana ni eneo la Jeshi la Magereza kuna sheria zake. 

Huu ni Mwanzo tuu wa Safari yetu lakini Maliasili zetu tutaendelea kuwapa matukio zaidi juu ya Mengi usiyo yajua 


 Kutoka kushoto ni Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango , Mzee Eliya na Fredy Anthony Njeje ambao walifika katika Kijungu na kujionea Mengi na ndio ambao wamewezesha Story hii kufika hapa kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu...

Toa Maoni yako au nini kifanyike ili kukuza utalii wa ndani kupitia simu namba +255 654221465

PICHA ZIMEPIGWA NA TONE MULTIMEDIA GROUP KUPITIA MTANDAO WA MBEYA YETU BLOG, SHUKURANI SANA KWAO

No comments:

Post a Comment