Social Icons

Tuesday, 28 October 2014

MALIASILI ZETU WATEMBELEA MAPOROMOKO YA KAPOROGWE NA KUJIONEA MENGI , IKIWA NI UTALII WA NDANI.

 Kama ilivyo ada Maliasili Zetu tumeamua kufanya mambo kwa Vitendo na si kwa maneno tuu.

Katika hili Tumeamua kuanza kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ambayo yanahusu maliasili zetu, utalii wa ndani na mambo ya Mazingira kwa ujumla.. 

Wiki kadhaa zilizopita tuliweza kuwaonesha Kijungu na mkajifunza mambo mengi sana kupitia hapo.

Leo ikiwa bado tupo Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Rungwe tunawaletea Maporomoko Maarufu ambayo kwa hakika kama haujawahi fika huko hii itakuwa ni nafasi yako ya kusafiri nasi moja kwa moja mpaka eneo ambapo maji yanamwagika na utajionea maajabu ya uumbaji wa Mungu.

 

Kwanza kabisa kabla haujapata Utamu zaidi hebu tuangalie Jinsi gani waweza fika hapo Kaporogwe.

Maporomoko haya ambayo yapo Kilometa 11 kutoka Ushirika Tukuyu sehemu ambayo kuna barabara nzuri na Gari la aina yoyote inaweza kufika katika kivutio hicho.

  Msimamizi (Admin) wa Mtandao huu alifika eneo Hilo na kujionea Mwenyewe eneo hilo na Maliasili hii na eneo ambalo kwa hakika linahitajika kusapotiwa na kulitangaza ili Dunia ipate fahamu kuwa kuna eneo kama hilo na wanahitaji kufika na Kutembelea.

Hivi ndivyo Safari yetu ilivyokuwa.. Fuatilia hapa 

Watu walikuwa wanajiuliza sana jinsi ya Kupita lakini ndio utalii wa Ndani
Hapa Msimamizi wa Mtandao huu wa Maliasili zetu akiwa anaelekea huko katika Maporomoko ya Kaporogwe
Unaweza ukastaajabu sana , Mto huu unaitwa Mto rangi kwa jina halisia , Jina la kaporogwe limekuja baada ya mtu mmoja aliyekuwa eneohili zamani za kale kudondoka katika maporomoko haya na Kuitwa Kaporogwe.  Maji haya ndiyo  yanaonekana yakitembea kwa kasi ndogo lakini ndiyo yanayoenda kumwaga maji yake katika maporomoko ya Kaporogwe.
Haya ndiyo Maporomoko ya Kaporogwe yanavyo onekana kwa ukaribu kabisa
 Hii ni njia yakuelekea Maporomoko ya Kaporogwe 
 Huu ni upande wa kuingilia kwa mbali ndivyo maporomoko yanavyo onekana 
 Hili ni Moja ya eneo la Mapumziko, watu wanaofika huja hapa na kukaa kisha kutazama uzuri wa Maporomoko ya Kaporogwe 
 Maji yakiwa yanashuka kwa kasi katika maporomoko ya Kaporogwe 
 Kwa Jirani kabisa Maji yanavyomwagika katika Maporomoko ya kaporogwe 
 Unaweza ukaona maajabu sana lakini hii ndio njia ya kuingilia maporomoko ya kaporogwe 
 Msimamizi wa Mtandao huu  Fredy Anthony Njeje akiwa chini kabisa ya Maporomoko ya Kaporogwe kujionea jinsi maji yanavyo mwagika, katika eneo hili la chini kuna hali ya unyevu vyavu na baridi ya aina yake ambayo haiumizi lakini inayohamasisha kuendelea kuwepo katika eneo hilo muda wote. hii ni Maliasili zetu ambapo tunafanya mambo kwa vitendo
 Hii ni Barabara inayotokea eneo Linaitwa Kissa kuelekea katika Maporomoko ya Kaporogwe  Wa kwanza kulia ni Fredy Anthony Njeje Msimamizi wa Mtandao wa Maliasili zetu  akiwa pamoja na wakazi wanaoishi maeneo ya Kaporogwe 
Hii ni Barabara nzuri ya Kuelekea katika maporomoko ya kaporogwe.
Na Maliasili zetu

No comments:

Post a Comment