Social Icons

Monday, 2 February 2015

ZITTO AMTAKA WAZIRI NYALANDU KUJIUZULU AKISHINDWA KUTOA TANGAZO GAZETINI LEO JIONI

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ifikapo leo jioni awe ametoa tangazo katika gazeti la serikali ili kuruhusu tozo mpya za mahoteli kwenye hifadhi la sivyo ajiuzulu cheo chake.

Sehemu ya ripoti inayoonyesha serikali inavyopoteza fedha nyingi kwa kukosa malipo ya tozo.
Zitto ameyasema hayo leo wakati akichangia kwenye majadiliano ya hoja za kamati bungeni.
Zitto amesema kuwa serikali inapoteza shilingi bilioni 2 kila mwezi kwa kitendo cha Waziri wa Utalii kutotoa tangazo katika gazeti la Serikali ili kuruhusu tozo mpya za mahoteli katika Hifadhi.Tangu mwaka 2011 mpaka 2014, Serikali imepoteza tshs 80 bilioni.

GLOBAL PUBLISHERS 

No comments:

Post a Comment