Social Icons

Tuesday, 14 April 2015

AKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI NGOZI YA CHUI NA NYUMBU


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mganga mmoja wa Jadi   kwa tuhuma za kumkamata akiwa na  ngozi mbili za chui na mkia wa nyumbu akiwa  amehifadhi  ndani ya chumba chake cha kulala
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri  alimtaja  mtuhumiwa  huyo aliyekamatwa  na nyara hizo za Serikali kuwa ni Kabichi  Nhulu (39)  Mkazi wa Kijiji cha Kakese   Tarafa ya Misunkumilo  Wilaya ya Mpanda Mkoani  hapa
 Alisema tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo lilitokea  hapo jana majira ya saa  kumi na mbili jioni nyumbani kwa mthumiwa katika Kijiji cha Kakese
 Alifafanua kuwa mtuhumiwa  huyo alikamatwa kufuatia taarifa   za kilizotolewa kwa jeshi la polisi kutoka kwa raia wema  kuwa  mtuhumiwa  huyo  anamiliki nyara za Serikali   visivyo  alali
 Alieleza baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi  lilifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya  upekuzi kwenye nyumba ambayo anaishi mtuhumiwa huyo
 Kidavashari alisema  baada ya polisi kufanya upekuzi ndani ya nyumba ya mtuhumiwa Kabichi   Nhulu alikamatwa akiwa na ngozi mbili za chui na mkia wa nyumbu akiwa amehifadhi ndani ya  chumba  chake cha kulala  akiwa ameficha chini ya  uvungu wa kitanda
 Mtuhumiwa  anaendelea  kushikiliwa na jeshi  la    Polisi  kwa mahojiano zaidi  na anatarajiwa kufikishwa   mahakamani  baada ya upelelezi  kukamilika  ili aweze kujibu tuhuma  inayomkabili


No comments:

Post a Comment