Social Icons

Saturday, 16 May 2015

WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO WAKIWA WAMEHIFADHI CHUMBANI KWA MWANAFUNZI‏

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Watu watatu wakazi wa Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  wanashikiliwa na jeshi la  Polisi Mkoa wa Katavi  kwa  tuhuma  za  kuwakamata  wakiwa na vipande vitatu  vya meno ya  Tembo  vyenye  uzito wa  kiligramu nane yenye thamani ya  zaidi ya shilingi  milioni kumi na moja
 Watuhumiwa hao waliokamatwa na meno hayo ya Tembo ni  Frank Hamisi(18)   Steven  Jonas (22) wakazi wa Kijiji cha Mnyaki A Makazi ya Wakimbizi  ya Katumba   na  Jackson  Erasto (34) Mkazi wa  kijiji cha Ivungwe   Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwaambia waandishi wa habari  kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana  majira ya saa tatu asubuhi  katika   eneo la kijiji  cha  Mnyaki A katika makazi ya wakimbizi ya Katumba
 Alisema watuhumiwa hao walikamatwa  kufutia taarifa zilizokuwa zimelifikia jeshi la Polisi  kutoka kwa Raia  wema kuwa  katika eneo   la Kijiji cha Mnyaki A  kwenye chumba  alichopangishwa  mwanafunzi  wa kidato cha nne wa shule  ya Sekondari ya Katumba aitwaye Evos   John(19)  kwenye nyumba  inayomilikiwa na  Felix  Gado  kuna meno ya tembo yalikuwa yamehifadhiwa na watuhumiwa  kwa ajiri ya kuyasafirisha  kwa Treani kutoka  Katumba  kuyapela Tabora
 Alieleza  kufuatia taarifa hizo  ndipo  Polisi  walipochukua hatua za haraka  za  kwenda kwenye eneo la Kijiji hicho cha Mnyaki A na kuizingira nyumba hiyo  waliokuwa wameitilia mashaka
Kidavashari  alieleza  ndipo upekuzi  ulifanyika kwenye  nyumba hiyo  na  viliweza kupatikana vipande vitatu vya meno ya Tembo  yenye uzito wa kilogramu nane  vyevye thamani ya Tsh 11,250,000 vikiwa  ndani ya chumba walikuwa wamelala  watuhumiwa hao  vikiwavimefungashwa  tayari kwa kusafirishwa
Katika  uchunguzi wa awali  umebaini  kuwa  watuhumiwa  kabla ya tukio la kukamatwa  walikuwa wameomba  kulala  katika chumba  cha mwanafunzi  Eno John kwa lengo la kusubilia  usafiri wa Treni  ya kutoka Mpanda kuelekea Tabora
Kamanda Kidavashari aliwaeleza waandishi wa habari kuwa    wanafunzi huyo aliwaruhusu watuhumiwa  kulala kwenye chumba chake  kwani walikuw a wakifahamiana  nao  kutokana na mahusiano ya kindugu  na hivyo  yeye siku hiyo  aliamua kuwaachia  chumba chake  na alikwenda  kulala kwa mwanafunzi mwenzake  jirani na hapo
 Mpaka sasa watuhumiwa hao waliokamatwa wanaendelea kushikiliwa  na jeshi la polisi  na wanatarajiwa  kufikishwa mahakamani   baada ya  upelelezi utakapo kuwa  umekamilika
 Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Katavi  ametowa wito  kwa jamii  kuachana  na tabia  ya kujihusisha  na biashara  haramu  ya nyara za Serikali  kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria

    

No comments:

Post a Comment