Social Icons

Tuesday, 9 June 2015

MKUTANO MKUU WA IDARA YA WANYAMAPORI TANZANIA WAFUNGULIWA JIJINI MWANZA.

Mkutano ukiwa unaendelea
 Picha ya pamoja Baada ya uzinduzi wa Mkutano huo

Mkutano mkuu Idara ya Wanyamapori Tanzania umefunguliwa leo tarehe 09 Juni 2015 na Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Msliasili na Utalii Ndg Selestine Gisimba utafanyika kwa mda wa siku 2 mpaka tarehe 12 Juni 2015.

Katika ufunguzi Naibu katibu mkuu aliwataarifu wadau wakati wa mkutano huu wajaribu kushauli kwa dhati namna gani ya kuhifadhi na hasa ukitilia manani mwaka huu ni wa uchaguzi ambao unaweza kuingilia katika utendaji wao wakazi.

Pia aliwambia kuna mambo mbalimbali ambayo yanafanya kuwepo na uongezeko la ujangili zikiwemo changamoto zifuatazo:

Ufinyu wa bajeti,uhaba wa vitendea kazi,uhaba wa watumishi,mmomonyoko wa madili miongoni mwa wafanyakazi.mambo yatakayo kua yameafikiwa yanatakiwa yawasilishwe wizaani kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Mkutano huu utahusisha wadau mbali mbali wa sctor ya wanyamapori wakiwemo wakuu wa mapori ya akiba,wakuu wa vikosi dhidi ya ujangili Tanzania vyuo vya wanyamapori na wadau wanaohusiana.

Mambo anayotarajiwa kujadiliwa ni Tarifa mbalimbali za wakurugenzi wasaidizi, Taarifa ya kamati ya kuboresha ukusanyaji wa Maduhuri, Hatua iliyofikiwa katika kuanzisha mamlaka ya Wanyamapori Tanzania, Uanzishwaji wa chama cha wahifadhi Tanzania, Utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mashirika ya kimataifa, Changamoto za utekelezaji wa Bajeti, Mikakati ya kuhifadhi Tembo waliopo katika Ranch za Kigoma,Kikurura,Mabale,Kitengule na msitu wa minziro nje ya Mapori ya kimisi,Burigi na Biharamulo.

Pamoja na hayo yote pia watajadili Nafasi ya Malihai club katika uhifadhi wa Wanyamapori

No comments:

Post a Comment