Social Icons

Wednesday, 29 July 2015

"MAJANGILI HAWAKUBALIKI NI JUKUMU LETU KUPAMBANA NA SWALA HILI" - HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWA MSIMAMIZI MKUU WA MALIASILI ZETU BLOG

"Ninasherekea Birthday yangu huku nikijifunga Mkanda kuanza hii Kampeni ya Kupambana na Majangili Nitasema .. Tutapambana mpaka Kieleweke.. Majangili hawakubaliki" Inaletwa kwenu na Mtandao wa Maliasili Zetu
Msimamizi wa Blog hii Fredy Anthony Njeje
Hivi karibuni Kupitia mtandao huu wa Maliasili zetu nimekuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi nimejionea mwenyewe Jinsi Tembo walivyo Pungua ma wengine wakiwa wanazaliwa bila kuwa na Mikonge ni kutokana na Mauaji ya wanyama hawa kuongezeka
 
Hii Sio Mikumi ile ambayo sisi sote tunaifahamu kwa undani kabisa.. Tembo hawa kwa hakika ni wachache sana, sababu kubwa ya kupungua ni hili swala la Ujangili na kuwamaliza kwa kasi Tembo hawa..

Ni jukumu letu sisi sote kupambana na Ujangili , kwanza kabisa tuanze na Tafsiri ya Ujangili kuwa ni Uchukuaji Haramu wa wanyama au Mimea ya Porini , na kuvunja sheria za eneo husika za Nchi ushirikiano ama za Kimataifa.

Shughuli hizi za ujangili ni pamoja na kuua wanyama wakati usio husika, na si muafaka , Kaika kusherekea Siku yangu ya kuzaliwa mimi msimamizi mkuu wa Blog hii ya Maliasili zetu pamoja na uongozi Mzima wa Blog hii Tumeamua sasa kwa nia moja kuanza kupigana , kupigania haki za wanyama na kupambana na Ujangili kwa Njia mbalimbali mpaka kuutokomeza kabisa.

Lakini kwa kuanza tuu wakati tunasherekea pamoja Sherehe hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa tujikumbushe ni wanyama wangapi wanakufa kila siku na kwa nini? 

Na majibu yake sasa yapo hapa kwamba ni lazima tuunge mikono kwa pamoja kupigana na ujangili , na hizi ni njia chache za kupambana na ujangili na kupunguza.

Kwanza kabisa unaweza kuripoti hali yoyote unayoitilia mashaka kuhusiana na wanyamapoli na makazi yao, yawapasa kuwa watoa taarifa Bora na wema kuhusiana na kitu chochote ambacho mnachokiona kinachohusiana na shughuli za ujangili

Kama upo eneo la Hifadhi au sehemu yenye Nyara za Serikali yawapasa mchange pesa kwa ajili ya kuchapisha vijarida au kuweka chapisho Gazetini ili watu wafahamu juu ya kutunza Nyara zetu.

Ingieni ubia na Taasisi za utafiti mbalimbali zinazohusika zikiwepo za vyuo vikuu kuangalia namna ya kujifunza kuendelea kutunza spishi ambazo zipo hatarini kupotea .

Andaa Matembezi ya nje yakionesha na kuweka wazi kutoweka kwa wanyama wa Porini.

Kwa hayo machache na ninaamini ya kwamba unaweza kuwa na mengi sana ya kupambana na Ujangili .. Basi sisi Maliasili zetu tunafungua milango kuungana nasi 

Mwisho kabisa Tunapenda kuwashukuru kabisa kipekee wadau wetu wote mnaotuunga mkono katika juhudi za kuendelea kufuatilia na kusoma Mtandao wetu  wa Maliasili zetu , Bila nyie sisi hatuwezi kuweka taarifa zozota hapa.. 

Wasiliana nasi kwa namba hii SMS, Whatsapp au kwa kupiga +255765056399 

Imetolewa na,
Uongozi
Maliasili zetu Blog

No comments:

Post a Comment