Social Icons

Friday, 20 May 2016

WAKUU WA MIKOA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

Kwa ufupi: Hifadhi ya Taifa ya Tarangire yenye ukubwa wa kilometa za mraba 2,850 iko umbali wa kilometa 118 kusini maghalibi mwa jiji la Arusha, Hifadhi hii ni maarufu kwa kuwa na makundi makubwa ya Tembo wanaoweza kuonekana katika eneo dogo na mengineyo mengi, Tujiunge hapa kuona Wakuu wa Mikoa walivyo Tembelea Hifadhi hii

Wakuu wa Mikoa wakiwemo wakuu wa wilaya waliowakilisha mikoa yao wakiwa katika ofisi za Shirika za Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kimafunzo katika Hifadhi ya TAifa ya Tarangire.


Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya wakiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire .

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa maelezo mafupi kwa Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya kabla ya kuanza safari ya kutembelea Hifadhi ya Tarangire.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara aliyekuwa mwenyeji wa wakuu wa mikoa hao,Joel Bendera akitoa neno la ukaribisho kwa wageni hao baada ya kufika katika Hifadhi ya Tarangire.

Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akichukua taswira wakati viongozi hao wakitembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyoko mkoani Manyara.

Kivutio kimojawapo ni Ndege katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.


Kundi la Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Wakuu wa mikoa wakitizama wanyama.

Mnyama Ngiri katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Tumbili na mtoto wake mgongoni katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.


Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya wakitizama eneo moja wapo la chanzo cha Mto Tarangire.

No comments:

Post a Comment