Social Icons

Saturday, 9 July 2016

KAMERA YA MALIASILI ZETU YAMULIKA BANDA LA MALIASILI NA UTALII VIWANJA VYA SABASABA NA KUJIONEA MENGI, UNGANA NASI HAPA

Msimamizi wa Blog ya Maliasili zetu Fredy Njeje akiwa katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kujionea yeye mwenyewe nini kilichokuwa kikiendelea katika banda hilo.
Hapa ni ndani ya Banda hilo la Maliasili na utalii ambapo kulikuwa na mambo mengi sana ya kujifunza 
Tukiwa ndani ya Banda la Maliasili na Utalii nilifanikiwa kuingia katika eneo la Malihai Club of Tanzania ambapo kwa bahati nzuri tulitembea na nyenzo zote hivyo kufanikiwa kujiunga na Kilabu hiki, na sasa Maliasili zetu ni wanachama wa Malihai. hapa nikikabidhiwa Majarida pamoja na kadi yetu na Ofisa wa wanyamapori bwana Said Mshana (Kulia) nyenzo ambazo kwa uhakika zitatusaidia katika kazi zetu za kutangaza utalii wa ndani na kuwafahamisha zaidi watu juu ya Maliasili zetu.
Hii ndio kadi Rasmi ya Malihai 
Baada ya Kumaliza Ziara yetu  tukatoka ma majarida pamoja na vitabu vya kutosha kwa ajili ya kujiendeleza zaidi.
Haya ni Baadhi ya 'Materials' ambayo niliyapata nilipotembelea Banda Wizara ya Maliasili na utalii
Picha zote na Maliasili zetu Blog

No comments:

Post a Comment