Social Icons

Monday, 29 January 2018

IDADI YA MATUKIO YA KUUAWA KWA TEMBO KATIKA HIFADHI YA KATAVI YA SHUKA.  Na  Walter  Mguluchuma .
         Katavi  .
  Idadi ya    ya  matukio ya kuuawa kwa  Tembo  katika   Hifadhi ya   Taifa  ya   Katavi  imeshuka  kutoka   tembo  24 kwa  mwaka  2016  hadi  kufikia   tembo     Tembo  watano  kwa  kipindi  cha  mwaka  2017 kufatia kuimarika  kwa  dolia   ndani ya  hifadhi  hiyo  na  nje ya  hifadhi .
    Hayo  yalisemwa  hapo  jana  na  Mkuu  wa   Hifadhi ya  Taifa  ya  Katavi   Izumbe   Msindai   wakati  alipokuwa   akizungumza  na   wandishi wa   habari  hapo  jana    Mkoani    Hapa .
Alisema   matukio   ya  kuuawa  kwa  tembo     ndani ya   Hifadhi ya  Taifa  ya   Katavi  yanaendelea   kushuka  kutokana  na kuimarishwa  kwa  dolia  na   ushirikiano  wanaopatiwa  na   wananchi  wanaizunguka  hifadhi  hiyo.
  Alifafanua  kuwa   kwa  kipindi cha  mwaka  2016 jumla ya  tembo   24 waliuawa    ndani  ya   hifadhi ya    Katavi na  kipindi  cha  mwaka 2017  tembo waliuawa ni  watano   na  kwa  mwaka huu wa  2018    kuna  tukio  moja  la  kuuawa kwa  tembo  mmoja   hadi  sasa .
   Alisema   hari ya   ujangili  ndani  ya   Hifaadhi  na  nje  ya   hifadhi   bado  ipo  kutokana   na   viashiria   hivyo   vya kuuawa   kwa  tembo  hao    katika   kipindi  hicho  cha  miaka   miwili  hivyo  matukio  hayo   hawaja yafumbia  macho .
  Msidai      alieleza  kuwa   hifadhi  ya   katavi   inakabiliwa  kubwa  sana ya   uongezeko la   mifugo   kuingia   ndani ya    Hifadhi  kwani       baadhi ya wafugaji wao  wanategemea  malisho ya mifugo yao  kwenye   maeneo  yaliohifadhiwa  wakati ni kinyume  cha    sheria .
  Alisema    kadri  siku   zinavyokuwa      zinaongezeka   na  ndio  matukio ya  kukamatwa  kwa  mifugo  ndani ya   hifadhi yamekuwa yakiongezeka  na  hasa   mifugo  inayohamishiwa     huku  kutoka  mikoa  ya   kanda ya  ziwa .
   Alitaja   aeneo  la    Wilaya  ya   Mlele  linalopakana   na   hifadhi  kwenye    Tarafa  ya   Mpimbwe  ndiko   kuna    changamoto   kubwa   sana   ya  mifugo  kuingia  ndani ya   hifadhi  na  wamekuwa wakiwachukulia  hatua  mbalimbali  wafugaji wanawakamata   akiwemo  kuwafikisha  mahakamani

No comments:

Post a Comment