Social Icons

Thursday, 1 February 2018

TAARIFA KWA UMMA : MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2018


TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2018
Tanzania pamoja na nchi wanachama wa  Mkataba wa Uhifadhi Ardhioevu (Ramsar Convention) inafanya maadhimisho ya siku ya ardhioevu duniani Fe kila mwaka. Ardhioevu ni maeneo yenye ardhi chepechepe yaliyopo kandokando na ndani ya Chemchemi, Mito, Maziwa na mwambao wa bahari wenye kina cha mita sita wakati wa kupwa. Ardhioevu pia hujumuisha Madimbwi, Mabwawa, Matingatinga na sehemu zote yanapokusanyika maji kipindi kirefu cha mwaka. Asilimia 10 ya ardhi ya Tanzania ni Ardioevu. Nchini kuna ardhioevu yenye umuhimu wa Kimataifa yajulikanayo kama Maeneo ya Ramsar. Maeneo ya Ramsar nchini yapo manne ambayo ni; Ziwa Natron yenye umuhimu wa kuhifadhi ndege aina ya Heroe Wadogo- (Lesser flamingo), Malagarasi Muyovosi  ina umuhimu wa kuhifadhi ndegemaji aina ya  Korongo Domokiatu (Shoebill Stork), Bonde la Mto Kilombero yenye umuhimu wa uhifadhi wa Puku na Rufiji mafia Kilwa uhifadhi wa Mikoko na Mazao ya Baharini.
Ujumbe wa mwaka huu ni: "Ardhioevu kwa Maendeleo Endelevu ya Miji”. Ardhioevu ni sekta endeshi ya uchumi wa nchi kwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika kwenye nyumbani, kilimo, uzalishaji wa umeme na uhifadhi wa wanyamapori ambao ni kivutio cha utalii nchini. Ardhioevu huzuia majanga ya mafuriko, hupunguza athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na madini hatarishi kama Zebaki.
Hata hivyo, ardhioevu nchini zinaharibika na zingine kutoweka kutokana na ongezeko la shughuli za kimaendeleo zisizo endelevu kama vile ujenzi kwenye vyanzo vya maji, ufugaji holela, kilimo kisichozingatia kanuni za kilimo cha kisasa na kukata miti ovyo. Athari zingine ni pamoja na vifo vya mimea maji na wanyama wanaotegemea maji kuishi na kunywa kutokana na matumizi yasiyoendelevu kama viboko, samaki na mamba.
Mamlaka inatoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Ardhioevu kushirikiana na Serikali kuyatunza maeneo haya kwa kutekeleza sheria mbalimbali za uhifadhi ikiwemo Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009, Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Sheria zingine za kisekta kama ya Maji na Uvuvi na kuwahimiza wale wote wanaoishi kwenye maeneo ya ardhioevu na hifadhi  kuhama sawa.

Imetolewa na,

MKURUGENZI MKUU
2 February 2018

No comments:

Post a Comment